Recent posts

View all
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo December 27, 2023
Club ya Simba imetangaza kuwasimamisha kazi Wachezaji wake wawili Nasoro Kapama na Clotous Chota Chama kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu.  Taarifa ya Simba imesema Wachezaji hao wawili pia wamepelekwa katika kamati ya nidhamu ya Simba SC kwa ajili ya hatua zaidi.  "Uongozi wa Club ya Simba unapenda kuwakumbusha Watumishi wake wote kuzingatia misingi ya maadili na nidhamu kwani haitosita kumchukulia hatua yeyote atakayethibitika kwenda kinyume na utaratibu huo" #SuluhutvUPDATES
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo December 5, 2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wamefika katika Kijiji cha Gendabi Kata ya Gendambi Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara eneo yalipotokea mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya Watu, majeruhi na uharibifu mkubwa wa miundombinu mbalimbali, yakiwamo mashamba na makazi ya Wananchi, leo December 04, 2023. #SuluhumediaUPDATES
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wamefika katika Kijiji cha Gendabi Kata ya Gendambi Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara eneo yalipotokea mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya Watu, majeruhi na uharibifu mkubwa wa miundombinu mbalimbali, yakiwamo mashamba na makazi ya Wananchi, leo December 04, 2023.  Viongozi hao wameongozwa na Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga kufika katika Kijiji cha Gendabi ambalo ni eneo lililoathirika sana na Maporomoko ya Matope kutoka Mlima wa Hanang yaliyotokea usiku wa kuamkia December 03, 2023.  Akiwa eneo la tukio hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista J. Mhagama, amewaomba Wananchi hao kupokea pole ambazo zinatoka kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambaye aliagiza lazima kufika eneo la tukio na kuona nini kifanyike kwa dharura kuhusu uokoaji pamoja na makazi kwa waathirika hao ambapo amesema Vikosi vinaendelea na uokoaji.  “Mambo haya yakitokea kuna mambo ya haraka yanatakiwa yafanyike kwa dharura hivyo tumekuja na kushauriana namna ya kujipanga kwa pamoja ili kufanikisha jambo hilo kwa uharaka”  Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kufungua miundombinu ya barabara inaendelea ili kurahisia kazi za uokoaji na kufikisha huduma muhimu za kijamii katika meneo yaliyoathirika “ Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS) tayari wamefungua barabara ya Singida-Babati ambayo awali ilikuwa haipitiki kutokana na kujaa tope na magogo ya miti kutoka milimani” #SuluhumediaUPDATES
Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kufuatia maafa yaliyotokea Kijiji cha Katesh Wilayani Hanang Mkoani Manyara leo na kusababisha vifo vya zaidi ya Watu 20 hadi sasa ambapo ametoa maelekezo kwamba nguvu zote za Serikali zielekezwe kwenye uokozi na kuzuia maafa zaidi kutokea.  Akiongea kutokea Dubai Rais Samia amesema “Kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa za kutokea kwa mvua kubwa Mkoa wa Manyara na kuleta madhara makubwa katika Kijiji cha Katesh, sisi tuliopo huku (Dubai) ambao tunashikiri mkutano wa mazingira tumesikitishwa sana na tukio hili lakini mipango ya Mungu ndivyo inavyokwenda tunatoa pole kwa Wahanga wa tukio hili”  “Nimeelekeza nguvu zote za Serikali zielekezwe huko kwenye uokozi na kuzuia maafa zaidi kutokea, Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama nimevielekeza vifike huko, Wizara ya Afya kushughulikia majeruhi lakini pia Wizara ya Madini kuona nini kinatokea katika sehemu ambayo Milima imeonesha kutetemeka au kuporomoka”  “Nimemtaka Waziri pia anayeshughulika na maafa awepo huko, niwape pole Wananchi wote nami nipo njiani kurudi huko kuja kushirikiana na Wananchi katika hili lililotupata” #SuluhumediaUPDATES
suluhu_media's profile picture #UPDATES Idadi ya vifo kutokana na mafuriko Wilayani Hanang imeongezeka kutoka Watu 47 (idadi ya jana) na kuzidi zaidi ya Watu 50 huku waliojeruhiwa wakifikia 85 na wengine wakihofiwa kufukiwa na tope baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha Wilayani humo ambapo juhudi za uokoaji zinaendelea.  Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus leo December 04,2023 imethibitisha kuongezeka kwa vifo hivyo ambapo imesema Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasssan anatoa pole kwa Wafiwa wote kutokana na msiba mkubwa uliowakumba na pia anawahakikishia Wananchi walioathirika kuwa Serikali iko pamoja nao na itahakikisha inashughulikia masuala yote yaliyotokana na janga hili.  “Kwa taarifa za awali nyumba na mifugo imeathirika sana huku idadi za kaya zilizoathirika ni 1,150, idadi ya Watu walioathirika hadi sasa ni 5,600 na pia inakadiriwa takriban ekari 750 za mashamba zimeharibika”  “Licha ya changamoto kadhaa zilizokuwepo uokoaji unavyoendelea ikiwemo barabara kuharibika huku tope na magogo kujaa barabara kuu a mitaani na kusababisha mawasiliano kukatika, Serikali inajitahidi kukabiliana nazo.  “Idadi ya vifo hadi sasa ni zaidi ya Watu 50 huku majeruhi waliopelekewa katika Hospitali mbalimbali za Wilaya, Mkoa na vituo vya afya ni zaidi ya 80” #SuluhumediaUPDATES