Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wamefika katika Kijiji cha Gendabi Kata ya Gendambi Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara eneo yalipotokea mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya Watu, majeruhi na uharibifu mkubwa wa miundombinu mbalimbali, yakiwamo mashamba na makazi ya Wananchi, leo December 04, 2023. Viongozi hao wameongozwa na Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga kufika katika Kijiji cha Gendabi ambalo ni eneo lililoathirika sana na Maporomoko ya Matope kutoka Mlima wa Hanang yaliyotokea usiku wa kuamkia December 03, 2023. Akiwa eneo la tukio hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista J. Mhagama, amewaomba Wananchi hao kupokea pole ambazo zinatoka kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambaye aliagiza lazima kufika eneo la tukio na kuona nini kifanyike kwa dharura kuhusu uokoaji pamoja na makazi kwa waathirika hao ambapo amesema Vikosi vinaendelea na uokoaji. “Mambo haya yakitokea kuna mambo ya haraka yanatakiwa yafanyike kwa dharura hivyo tumekuja na kushauriana namna ya kujipanga kwa pamoja ili kufanikisha jambo hilo kwa uharaka” Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kufungua miundombinu ya barabara inaendelea ili kurahisia kazi za uokoaji na kufikisha huduma muhimu za kijamii katika meneo yaliyoathirika “ Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS) tayari wamefungua barabara ya Singida-Babati ambayo awali ilikuwa haipitiki kutokana na kujaa tope na magogo ya miti kutoka milimani” #SuluhumediaUPDATES
0 Comments