suluhu_media's profile picture #UPDATES Idadi ya vifo kutokana na mafuriko Wilayani Hanang imeongezeka kutoka Watu 47 (idadi ya jana) na kuzidi zaidi ya Watu 50 huku waliojeruhiwa wakifikia 85 na wengine wakihofiwa kufukiwa na tope baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha Wilayani humo ambapo juhudi za uokoaji zinaendelea. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus leo December 04,2023 imethibitisha kuongezeka kwa vifo hivyo ambapo imesema Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasssan anatoa pole kwa Wafiwa wote kutokana na msiba mkubwa uliowakumba na pia anawahakikishia Wananchi walioathirika kuwa Serikali iko pamoja nao na itahakikisha inashughulikia masuala yote yaliyotokana na janga hili. “Kwa taarifa za awali nyumba na mifugo imeathirika sana huku idadi za kaya zilizoathirika ni 1,150, idadi ya Watu walioathirika hadi sasa ni 5,600 na pia inakadiriwa takriban ekari 750 za mashamba zimeharibika” “Licha ya changamoto kadhaa zilizokuwepo uokoaji unavyoendelea ikiwemo barabara kuharibika huku tope na magogo kujaa barabara kuu a mitaani na kusababisha mawasiliano kukatika, Serikali inajitahidi kukabiliana nazo. “Idadi ya vifo hadi sasa ni zaidi ya Watu 50 huku majeruhi waliopelekewa katika Hospitali mbalimbali za Wilaya, Mkoa na vituo vya afya ni zaidi ya 80” #SuluhumediaUPDATES
0 Comments